Kimashami, Kamusiya Kigogo-Kiswahili-Kiingerezai, Rugemalira J., 2008

Kimashami, Kamusiya Kigogo-Kiswahili-Kiingerezai, Rugemalira J., 2008.     

Ingawa kuna maandiko kadhaa katika lugha ya Kimashami, kamusi hii ni ya kwanza kuandaliwa kwa lugha hii. Kamusi yenyewe imekusudiwa kukidhi mahitaji ya wasomaji wa aina mbili. Kwanza, kama ilivyokusudiwa katika mpangilio wa Mradi wa Lugha za Tanzania, itakidhi mahitaji ya watafiti wa isimu wanapofanya uchunguzi kwa kulinganisha data za lugha mbalimbali. Pili, katika jitihada za kukuza na kuhifadhi lugha za Tanzania, kamusi hii itakidhi mahitaji ya msomaji wa kawaida, hasa yule ambaye lugha yake ya kwanza au lugha ya kwanza ya wazazi wake ni Kimashami. Inatazamiwa kwamba kamusi hii itaweka msingi wa kutengeneza kamusi sanifu ya Kimashami, na kuimarisha vigezo vya tahijia na maandishi kwa jumla katika lugha hii.

Kimashami, Kamusiya Kigogo-Kiswahili-Kiingerezai, Rugemalira J., 2008


Shukrani.
Shukrani za dhati ziwaendee watu wote katika sehemu mbalimbali za wilaya ya Hai kwa kutoa msaada wa hali na mali wakati wa utafiti kwa ajili ya uandaaji wa orodha hii mwezi Agosti na Septemba 2004: Mwalimu Asantaeli Kweka wa Nshara, Mwalimu Mave Mfuru wa Nkwarungo, walimu wote wa shule ya msingi Nshara Ufundi, Mzee Godwin Kimbita wa Masama, walimu wote wa shule ya msingi Mweeki, Bwana Barakaeli Mmari na Bwana Justo Mbasha wa Hai Bomani, Bwana Elineema Kimaro (Afisa Utamaduni wa Wilaya).



Бесплатно скачать электронную книгу в удобном формате, смотреть и читать:
Скачать книгу Kimashami, Kamusiya Kigogo-Kiswahili-Kiingerezai, Rugemalira J., 2008 - fileskachat.com, быстрое и бесплатное скачивание.

Скачать pdf
Ниже можно купить эту книгу по лучшей цене со скидкой с доставкой по всей России.Купить эту книгу



Скачать - pdf - Яндекс.Диск.
Дата публикации:





Теги: :: :: :: :: ::


Следующие учебники и книги:
Предыдущие статьи:


 


 

Книги, учебники, обучение по разделам




Не нашёл? Найди:





2025-01-22 04:34:54